Karibu katika blog ya G4D TZ REAL. Tangaza nasi biashara,matangazo,kazi na muziki wako hapa kwa bei nafuu sana wasiliana nasi kwa simu no. 0625910376 au WhatsApp no. 0755317537 Asante

Millionaire  Ads

Fainali ya tatu Argentina wanaondoka bila Kombe, Chile Bingwa wa Copa America


Alfajiri ya June 27 2016 ndio ilikuwa siku ambayo mashabiki wa soka la bara la America macho na masikio yao yote yalikuwa New Jersey Marekani katika uwanja wa MetLife, lengo na shauku kubwa ilikuwa ni mashabiki kushuhudia fainali ya Copa America 2016 ambayo ilikuwa inazikutanisha timu za Argentina dhidi ya Chile.
Huu ulikuwa ni mchezo wa pili mfululizo kwa Chile na Argentina kukutana katika hatua ya fainali ya michuano hiyo, Chile wameiadhibu Argentina kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya dakika 120 kumalizika kwa sare ya 0-0, Argentina wameonekana kutokuwa na bahati, kwani nahodha wao Lionel Messi alikuwa ni miongoni mwa wachezaji waliokosa penati.


 Hii ni fainali ya tatu mfululizo timu ya taifa ya Argentina inakosa Ubingwa, ilikosa Ubingwa wa Kombe la dunia 2014 dhidi ya Ujerumani, ikakosa taji la Copa America 2015 katika hatua ya fainali dhidi ya Chile na leo June 27 imepoteza tena mchezo wa fainali kwa mara ya pili mfululizo dhidi ya Chile.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Millionaire  Ads

.

Copyright © 2017 G4D MEDIA