Hot Posts

Hizi Ni Picha 6 Za Bei ya jezi za nyumbani za Man United watakazovaa 2016/2017


Baada ya Man United kutambulisha jezi zao za ugenini zenye rangi ya blue watakazotumia katika msimu wa 2016/2017, leo Jumamosi ya July 23 Man United wametambulisha rasmi tena jezi zao mpya watakazotumia katika mechi za nyumbani.


 Jezi za nyumbani za Man United huwa na rangi nyekundu utofauti huwa ni muundo tu, Man United kwa sasa jezi zao zitakuwa na rangi nyekundu iliyokolea upande mmoja na upande pili rangi nyekundu iliyopooza, kama utakuwa unahitaji jezi ya Man United ya mikono mifupi bila jina na namba ni pound 60 ambazo ni zaidi ya Tsh 170000.


 Kwa upande wa mashabiki watakaopenda kuvaa jezi za nyumbani za Man United za mikono mirefu watalazimika kulipa pound 65 ambazo ni zaidi ya Tsh 180,000, bukta pound 30 ambazo ni zaidi ya Tsh 80,000, soksi pound 13 ambazo ni zaidi ya Tsh 35,000, kwa watakaopenda kuvaa full itakuwa pound 103 ambazo ni zaidi ya Tsh 290,000.
No comments