Hot Posts

Tazama Jinsi Rekodi ya Man United iliyodumu kwa miaka 8 imevunjwa na FC Bayern


Usiku wa Spetemba 13 2016 tulishuhudia mechi za ufunguzi za michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini mashabiki wa soka hawakuishia kuangalia mechi za ufunguzi ilikuwa ni siku pia ya kuona rekodi kadhaa zikivunjwa na kuwekwa.
Staa wa FC Barcelona Lionel Messi amevunja rekodi mbili zilizokuwa zinashikiliwa na Cristiano Ronaldo, rekodi ya kufunga hat-trck nyingi katika michuano ya UEFA Champions League kwa kufunga hat-trick ya 6, hata hivyo ushindi wa goli 5-0 wa FC Bayern Munich dhidi ya FK Rostov ulivunja rekodi ya Man United iliyodumu kwa miaka 8.
FC Bayern Munich wamevunja rekodi ya Man United ya kufunga mechi 12 mfululizo za Ligi ya Mabingwa Ulaya katika uwanja wao wa nyumbani kwa kufunga mechi ya 13 jana dhidi ya  FK Rostov, rekodi ya Man United iliwekwa kati ya mwaka 2006 hadi 2008 na imevunjwa jana na FC Bayern baada ya kuibuka na ushindi wa goli 5-0.
Mechi 13 walizoshinda FC Bayern na kuvunja rekodi ya Man United
1- Septemba 13 2016 vs Rostov 5-0
2- May 3 2016 vs Atletico Madrid 2-1
3- April 5 2016 vs Benfica 1-0
4- March 16 2016 vs Juventus 4-2
5- November 24 2015 vs Olympiakos 4-0
6- Novemba 4 2015 vs Arsenal 5-1
7- Septemba 29 2015 vs Dinamo Zagreb 4-0
8- May 12 2015 vs Barcelona 3-2
9- April 21 2015 vs Porto 6-1
10- March 11 2015 vs Shaktar Donetsk 7-0
11- December 10 2014 vs CSKA Moscow 3-0
12- Novemba 5 2014 vs Roma 2-0
13- Septemba 17 2014 vs Manchester City 1-0

No comments