Hot Posts

Hot Newz : Leo Alikiba kakabadhiwa Tuzo yake ya MTV EUROPE


Mwimbaji staa wa bongofleva Alikiba leo Johannesburg South Africa amekabidhiwa tuzo yake ya MTV EURO aliyoshinda baada ya tuzo hiyo kutolewa kimakosa kwa Mwimbaji staa wa Nigeria Wizkid.
November 2016 MTV EUROPE walitoa tamko kwamba tuzo hiyo aliyestahili kupewa alikua ni Alikiba ambaye mpaka muda wa mwisho kwenye utoaji tuzo ndio alikua anaongoza kwa kupigiwa kura nyingi na Mashabiki mitandaoni.Baada ya November 2016 kutangazwa kwamba itachukuliwa kwa Wizkid ili apewa Alikiba, leo February 17 2017 ndio Alikiba amekabidhiwa na MTV kwenye mji wa Johannesburg Afrika Kusini ambapo baada ya kukabidhiwa ameongea machache yafuatayo.

Hii ni Tuzo yetu, tumeipigania na tumeipata…. asanteni sana kwa kunipigia kura, namshukuru Mungu pia kwa baraka zake, familia yangu, Management yangu na mashabiki”Alikiba

No comments